Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Saturday, November 8, 2014

Mgambo na Coastal Mambo si mambo

Matokeo ya Mwisho
Wachezaji Mgambo

Yanga
 Ligi kuu ya soka Tanzania Bara VPL Jana iliendelea katika viwanja mbali mbali Nchini huku ikishuhudia timu mbili kutoka Tanga za JKT Mgambo na Coastal Union Wagosi wa Kaya wakiingia Dar-es-salaam na kucheza mechi zao kwa siku moja,Mgambo JKT Wao walikuwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kuwavaa Yanga africa mechi ambayo ilitafsiriwa kaa ni ya kulipa kisasi kwa Yanga kwani katika Msimu uliopita Yanga walipoteza matumaini ya Ubingwa baada ya Kuchapwa na Mgambo pale mjini Tanga kwa mabao 2-1 hivyo kuacha mbio za ubingwa kuwa za Upande mmoja tu wa Azam.
Akili na Fudu
Cholo,Maganga na Busungu
 Mechi ilianza kwa kasi sana huku kila timu ikiwa na Shauku ya kuanza kufunga Goli lakini haikuwa hivyo kwani mpaka mapumziko timu zilitoka bila kuona Mlango wa mwengine,Kipindi cha pili kilianza kwa Kasi lakini maamuzi ya Refa kutoa kadi Nyekundu kwa Kipaga kulivuruga Mipango yote ya Mgambo JKT Kwani iliwavuruga kwa Muda huo.Mgambo Shooting kupitia kwa Balimi Busungu ambaye alionekana kuichachafya Ngome ya Yanga aliingia kwenye Boksi na Kuangushwa ambapo kikawaida ilikuwa iwe ni kadi Nyekundu na Penalt hata hivyo Refa alifumbia macho.Yanga walipata Bao ambalo lililalamikiwa na kila shabiki kwani lilikuwa Offside kupitia kwa Mchezaji wake Simon Msuva,Goli hilo lilipelekea kuwachanganya zaidi Mgambo lakini walijipanga na kufanya mashambulizi kutafuta magoli ya kurudisha

Shime akikumbatiwa na Maximo
 Mgambo waliwaingiza Kibakuli,Gila na Malima ili kuendeleza mashambulizi ya Kurudisha Goli hilo lakini bila mafanikio ilikuwa Yanga tena walioandika bao la pili kupitia kwa Msuva tena na hadi firimbi ya Mwisho Yanga 2 Mgambo shooting bila..kwengineko kule Chamanzi Wagosi wa Kaya Coastal union walichapwa na wenyeji wao Azam FC Kwa kipigo cha mabao 2-1 na kuendeleza Rekodi mbaya kwa Coastal kwani mara nyingi hawapati matokeo mazuri,magoli hayo yalipatikana ndani ya dakika tano kwa Uzembe wa mabeki wa Coastal kutokuwa makini.
Maximo
Ligi hiyo itasimama kupisha mashindano ya uhai ya Vijana pamoja na Chalenge kwa Timu ya Taifa
Bakari Shime na Muamuzi wa AKIBA

Captain wa Yanga Kiiza AKIHOJIWA

SALVA Akitoa maelezo

heka heka

Timu zikiingia

Mashabiki yanga

Coutinho

basi la Yanga

Twite na Coutinho

Mgambo kabla mechi haijaanza

akili na Coutinho

Kiiza akijiandaa kuingia

No comments:

Post a Comment