Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Wednesday, November 5, 2014

Mashabiki Mbeya Waacha Mbachao

Wenyewe wana kamsemo kao Mbeya Kwanza,
Mashabiki wa Mbeya City ama Wakazi wa Mbeya
na Vitongoji vyao wameibukia kuwa washabiki
wazuri wa Mpira wa Miguu kwa sasa Nchini hadi
kufikia kutunga hako kamsemo Mbeya kwanza
wakimaanisha kuwa watashabikia Mbeya City
kwanza si Yanga wala Simba,Ila mimi naona ni
wanafiki tu kwani wao wao ni mashabiki wazuri
wazuri wa Timu hizo zenye Utani wa Jadi Nchini,
Mada yangu ya Leo ilikuwa kuhusu Mashabiki wa
kutoka Mbeya walivyoacha Mbachao kwa Msaada
upitao"Msaada Upitao nazungumzia Mbeya City"
Timu hii Tokea Kuanzishwa kwake ina Miaka Minne
tu ama mitano na Ligi kuu ina Miaka 2 tu,Msimu
wa Kwanza waliwateka sana watu wa Mbeya

Mashabiki
Mpaka kufikia kuanzisha hako kamsemo Mbeya kwanza,lakini Msimu huu naona mambo yanawaendea Kombo hadi kufikia kutaka kumtimua Kocha wao Juma Mwambusi.Bado sijaongelea hii mada ila naomba pia nielezee Mbachao ni nini?Mbachao ni Tanzania Prisons ya Mjini Mbeya pia timu ambayo ina takribani zaidi ya Miaka Kumi kwenye Ligi kuu Tanzania Bara bila Kutetereka isipokuwa Msimu uliopita,Zikitajwa Timu vigogo Tanzania na Kongwe ama kwa hakika Prisons ya Mbeya itakuwepo bila shaka,Iliibeba sana Mbeya kwa Muda mwingi ambao timu kama Tukuyu Stars na MECCO Zimeshuka daraja wao ndio walikuwa wamekuwa walezi wa mashabiki Mjini Mbeya,
lakini kwa sasa inasikitisha Prisons haithaminiwi
tena Mbeya kama ilivyo awali kisa Mbeya City
kuingia ligi kuu,Msimu uliopita ulikuwa Mbaya
kuliko misimu yote kwa Tanzania Prisons kwani
ilifikia kucheza Mtoano na Ashanti united kutoka
Dar na Shukrani mchezo ulichezwa kiwanja cha
Jmahuri Morogoro na kuifanya Tanzania Prisons
kubakia Ligi kuu kwa kuwafunga Ashanti United,
Mashabiki Mbeya City

Mashabiki wa Coastal Wakiishangilia Mgambo Shooting
Katika mbio za Tanzania Prisons kujinusuru
kushuka Daraja Njiani walikutana na Mbeya
          City katika Uwanja wa Sokoine cha ajabu
          Hakuna Sapoti yoyote kutoka kwa mashabiki
          kuishangilia Tanzania Prisons angalau Ibaki
          Ligi kuu hapa ndipo linakuja swala la unafiki
          wa watu wa Mbeya,Mnasemaje MBEYA kwanza
          halafu mnataka Tanzania Prisons Ishuke Daraja?
Mashabiki Mbeya City wakiomba Dua Mkwakwani
Mmesahau jinsi timu hii ilivyowaletea Burudani kwa
kipindi kirefu cha kutokuwepo kwa timu yoyote
shriki ya ligi kuu Tanzania Bara?Leo imekuwa haifai?
Mimi nawapenda sana mashabiki wa Tanga,
Inajulikana na inaeleweka hakuna Mshabiki wa Mgambo
shooting na hata tokea,iko wazi ni timu ya taasisisi kama
Tanzania Prisons,Lakini ikifikia saa Mgambo wanahitaji
Support mashabiki wanaitikia wito,Mwaka Jana Mgambo
walikuwa katika hali kama waliyoipata Tanzania Prisons
na walikuwa na Mechi ngumu sana dhidi ya Simba,
Mtibwa,Azam na Yanga Mkwakwani,Mechi dhidi ya
Yanga mashabiki walidiriki kumtishia Refa ili asiwaume
Mgambo na isishuke daraja kwani watu wanajua thamani
ya timu zao hapa Jijini,Mashabiki wa Tanga Wengi wao
ni African Sports na Coastal union,lakini kwa ajabu ya
Mungu wote waliungana Kuipigania Mgambo Isishuke
Daraja lakini Mbeya Prisons katokea Tundu ya Sindano.
Mashabiki Mbeya City wakiitania Mgambo Shooting
Hakuna aliyejali matokeo ya timu hiyo hata kidogo kule Mbeya
lakini ukiwauliza watakwambia Mbeya Kwanza,Mbeya ipi hiyo
          ambayo Tanzania Prisons Hakai?Mimi kama Mimi Nawashauri
          Viongozi wa Tanzania Prisons Kuihamisha Hiyo timu Mbeya kwani
          Inasikitisha kucheza Nyumbani kama Ugenini,Waacheni wananchi wa
          Mbeya na Unafiki wao wa Mbeya kwanza.KILA LA KHERI TANGA
          NA TUNASEMA TUKIWA KIFUA MBELE TANGA KWANZA
Mashabiki Coastal Union wakiishangilia Mgambo

Mashabiki Coastal Wakiizingira Gari ya Mbeya City

No comments:

Post a Comment