Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Monday, November 3, 2014

Mgambo waiduwaza Mbeya City

Bango la Matokeo
 Timu ya soka ya Mgambo shooting ya Tanga leo imewaduwaza Mbeya City kwa kuwafunga magoli mawili kwa Moja katika Mchezo safi na Wa kuvutia Uliofaanyika katika Uwanja wa Mkwakwani,Magoli ya Mgambo yaliwekwa Kimiani na Busungu kwa Njia ya Penalt baada ya walinzi wa Mbeya City kumkwatua Nassoro Cholo katika eneo la hatari,hivyo muamuzi kuamuru ipigwe Penalt ambayo Busungu bila ajizi aliiweka kimiani.Mchezo huo ambao ulikuwa wa kuvutia lakini Mgambo shooting ni wa Kujilaumu wenyewe baada ya Kukosa mabao takribani saba ya wazi katika vipindi vyote viwili,
Kikosi cha Mgambo
 Mgambo waifanikiwa kupata bao la pili kupitia Ally Nassoro FUDU Kutoka umbali wa mita 22 alilopikiwa na Busungu baada ya kuwatambuka mabeki wa Mbeya City.Mchezo huu awali ulikuwa ufanyike jana ila kutokana na Mvua kubwa iliyonyesh jijini hapa ulishindikana kufanyika hivyo kuwapa mashabiki wa Mbeya City wakati Mgumu kwani hawakuwa na Bajeti ya Kulala Jijini Tanga.Timu ya Mgambo wiki hii inatarajiwa kwenda kucheza na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam.Kila la Kheri Mgambo shooting Club
PERA KAZINI

Ali Nassoro na Peter Malianza wa Mbeya City

Macaptain na Marefaree

Kocha wa Mgambo Bakari Shime Nyundo(BLACK WIZARD)

Mashabiki wa Coastal wakiisuport Mgambo

Chico kazini

Watu kazini

Kikosi cha mbeya City

Fulmence MAGANGA Captain wa Mgambo

Full maganga KAZINI(MAN OF THE MATCH)

Busungu Mfungaji wa Goli la Kwanza

ajali kazini

Ali nassoro akishangilia

No comments:

Post a Comment