MSHAMBULIAJI Radamel Falcao yuko tayari kuongeza nguvu kikosini Manchester United katika mechi dhidi ya Hull City Uwanja wa Old Trafford Jumamosi baada ya kupona maumivu yake.
Nyota
huyo wa Colombia amekuwa akisumbuliwa na maumivu tangu amejiunga na
United kwa mkopo kutoka Monaco msimu huu na hajacheza kwa wiki tano
sasa.
Lakini
kocha Louis van Gaal amesema Falcao anajiandaa kurudi kikosini mwishoni
mwa wiki hii, na Marcos Rojo anaweza pia kuorodheshwa baada ya kupona
maumivu ya bega aliyopata katika mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester
mwanzoni mwa mwezi huu.
Manchester United wametweet picha hii ya Falcao kurejea mazoezini wiki hii 

Beki Marcos Rojo pia amerejea baada ya Kuwa Nje kwa Muda
No comments:
Post a Comment