KLABU ya Arsenal inakabiliwa na baa la majeruhi, baada ya Jack Wilshere naye kutakiwa kuwa nje kwa miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu jana.
Na
kocha Arsene Wenger atalazimika kuingia sokoni Januari kununua
wachezaji ili kupoza maumivu ya tatizo la majeruhi kikosini mwake.
Wilshere
amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto baada ya kipigo
cha Manchester United cha mabao 2-1 Uwanja wa Emirates Jumamosi
iliyopita. Na Nahodha, Mikel Arteta pia anaweza asicheze tena mwaka huu
baada ya kuumia Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund.

Wilshere ameposti picha hii baada ya kufanyiwa upasuaji
Kuuminia kwa Wilshere kunamfanya kocha Arsene Wenger awakose viungo wote watatu tegemeo, Aaron Ramsey, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky.
Baada ya upasuaji huo, Wilshere akaposti picha Instagram akiwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba zoezi limekwenda vizuri.
"Kifundo cha mwishowe kilihitaji upasuaji," ameandika. "Zoezi limekwenda vizuri na asante kwa mkuu James Calder (mpasuaji)!

Wilshere akiugulia maumivu baada ya kuumia na anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kabla ya Machi, mwakani
No comments:
Post a Comment