![]() |
| Nizar Khalfan Akikabana na Mario Baloteli |
![]() |
| Mrisho Ngasa akikabana na Rafael |
![]() |
| Abdulrahaman Humud akikabwa na Wabrazil |
Kisa hiki nakifananisha na Mastaa wetu wa Soka la Bongo ambao wanaenda kujaribu bahati yao ya kucheza soka Nje ya Nchi hakuna hata mmoja anayekuja na maneno yaliyonyooka,kila mmoja anakuja na maneno yasiyoeleweka hivyo kuwaacha wapenzi na wadau wa Soka wasijue wapi pa Kuanzia kufuatilia ama Nini kinahitajika kwa mwanasoka kwenda Kucheza soka Nje,matokeo yake kama kukosea tunaendelea kukosea tu kila mara,Kwa Tanzania ukiambiwa uwataje wachezaji kumi wazuri Zaidi kuwahi kutokea Usipolitaja Jina la Edibily Jonas Lunyamila utakuwa Unafanya Kusudi tu ama umesahau ama Hujui soka letu vyema,Akiwa katika kilele cha soka lake alibahatika kwenda Nchini Ujerumani kwa majaribio katika timu ya FC KOLOGNE ya nchini humo,kilichotokea akaibukia katika Mechi ya watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga pale Mjini Mwanza na asiwe na maelezo ya kina kuelezea nini kilimsibu akiwa kule,watu wakasema tatizo Uzito wake mdogo wengine wakasema kaambiwa aende timu ya madaraja ya Chini kwanza kuinua kiwango ilimradi kila mtu kasema yake,mwishowe akahitimisha kisa cha mtema kuni ambae hadi leo haijulikani alioana nini porini kiasi cha kufia katikati ya kijiji mwenyewe,Tazama Mchezaji kama Golikipa wa Zamani wa Wagosi wa Kaya na Simba Sports Club na Timu ya Taifa aliyepewa Jina la Tanzania One Mwameja Mohamed Mwameja,aliondoka Nchini kuelekea Africa Kusini kuchezea Jomo Cosmos yay a Huko,baada ya kipindi kifupi tukasikia yuko Nchini Uingereza katika Timu Ya Reading akifanya majaribio lakini pia hapo hapo kuna waliosema alikuwa anachuma matunda,Wapenzi wa Soka hawakupata Jibu la maana la nini kilichoendelea kwa Mohamed Mwameja,akajirudia Nchini Maisha yakaendelea.Kuna Huyu Nizar Khalfani ambaye alikuwa anakipiga katika timu ya Vancover white cape ya Canada kwa Miaka kadhaa na akafanikiwa kucheza ligi
ya marekani..major soccer league,Amerejea nchini
bila maelezo ya kutosha kuhusu nini kimemsibu
huko,kwani ki uhalisisia huwezi fananisha major
soccer League na ligi ya Bongo,kuna tatizo hapa.
![]() |
| Mrisho Ngasa na Gianfranco Zola |
Tazama Mchezaji kama Mrisho Khalfani Ngasa,kwangu mimi ni mchezaji Bora sana kuwahi kutokea hapa Nchini kwa Kipindi cha Takribani Miaka kumi,Alipata bahati ya Kuenda Kujaribiwa Westham United Kule nchini Uingereza hali iliyoibua Furaha kubwa sana kwa mashabiki wa soka la Bongo kwa kuona sasa tutaanza kupaa katika medani ya kimataifa,aliporudi kutoka kwenye majaribio kila mmoja alisema lake nay eye mwenyewe pia hakuwahi kunyoosha maneno,ni kama yule mtema Kuni kule katika kijiji cha kufikirika,hatukukaa sawa Mrisho Ngasa huyu huyu akaitwa Settle Sounders ya Marekani kwa Majaribio tena..huku ndio ilikuwa Balaa Zaidi kwani alijaribiwa na Kucheza Mchezo wa Kirafiki Dhidi ya Manchester United ya Kule England.ina maana alipata bahati ya kuonekana na watazamaji kote Duniani,kilichotokea baada ya hapo akarudi Tanzania na kuendelea na soka la Bongo,Bado Mrisho khalfani Ngasa huyu huyu alitakiwa kununuliwa na EL Merekh ya Sudan bila ya majaribio lakini jambo lililofanya Ngasa asiende kule ni kitu gani bado ni Kitendawili pia Mpaka leo,na Kuhitimisha Kisa cha Mtema Kuni kwa Mrisho Khalfani Ngasa.Tazama Shomari Kapombe,huyu alichukuliwa hapa kwenda kwenye majaribio Ufaransa,amekaa huko kwa kipindi kirefu sana na Watanzania walikuwa na Imani sana nay eye,Kilichotokea alirejea kwa ajili ya kuichezea Timu ya Taifa halafu zikabakia Hadithi,hajatumiwa Nauli..oohh anaumwa malaria,yeye mwenyewe akitafutwa hataki kuongea kitu anasema amepumzika sasa maswala ya soka na hataki Bughudha mwishowe kaibukia AZAM FC na maisha yanaendelea na Kisa cha Mtema kuni kama kawaida kinashika hatamu tena....
![]() |
| Mbwana Samata na Wacameroon Kazini |
Tazama Huyu mwengine Haruna Moshi Boban,alipata bahati ya kusajiliwa na Kuchezea timu ya ligi kuu kule Denmark,kilichotokea baadae alirudi Bongo na wakala wake nayeye wakawa wanapishana maneno ya kuwaambia wapenzi mashabiki Nchini,kwa kifupi hakuna aliyeelewa nini ilikuwa tatizo kwake mwishowe Simba wakachukua Mchezaji wao,baadae Wagosi nao wakamsajili na Kisa cha Mtema Kuni kilishika mkondo kama kawaida yetu,Orodha ni ndefu sana Kuanzia kwa Renatus Njohole,Subday Manara,Henry Joseph shindika na Nizar Khalfan wote hawa waliwahi kuenda Ughaibuni na kuturejea na Majibu yasiyoridhisha kama yule mkata kuni aliyekufa katikati ya kiji cha kufikirika,kwa kumalizia Kuna hawa wawili Tegemeo letu Taifa Stars kwa sasa,
![]() |
| Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu T.P MAZEMBE |
Thomas Ulimwengu na Mbwana Sammata hawa nao kuna dalili ya kutuletea Kisa kile kile cha Mtema Kuni,kwani hakuna anayejua nini kinawasibu huko Zaidi ya kushukuru mungu kuona wanacheza,lakini kufikia mwisho wa safari Nchini Congo bado haitoshelezi ki ukweli,tunawatarajia tuwaone wanaenda mbali Zaidi ya pale kwani soka lao linaruhusu,Umri una ruhusu na taya Experince ya soka la nje wanalo la Kutosha sio kama hawa kina Ngasa wanaotokea hapa kwenda nje na kurudi heri wao watokee nje kwa nje inaweza kuwa rahisi kwao..
![]() |
| Mwameja Mohamed Mwameja |
![]() |
| Mrisho Khalfani Ngasa |
Wito wangu kwa wanasoka wetu wawe na Kiu ya mafanikio na pia
wawe na Tabia ya kusema ukweli pindi wanaporudi,majaribio alishindwa Van
Nesterooy Manchester United kwa mara ya Kwanza ije kuwa sisi wa Tanzania
huku,Ukisema ukweli Itakusaidia kama sio wewe Mwanao kwani Soka letu ndio hili
hili,








No comments:
Post a Comment