Timu ya soka ya Coastal Union Wagosi wa kaya,jana waliifanyia kitu Mbaya Ruvu shooting ya Mabatini kibaha kwa Kuichachafya katika mchezo wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara.
Wanajeshi hao walioingia Tanga wakiwa na kumbukumbuku nzuri ya kuwachapa Azam bila huruna pale Chamazi,lakini jana hawakufua dafu mbele ya wagosi wa kaya Coastal union waliokuwa wanachagizwa na mashabiki lukuki waliohudhuria pambano hilo.
 |
| Yusuph Chuma Akisubiria Kuingia |
Iliwachukua Kipindi kizima cha kwanza kwa Mpira kuchezwa upande mmoja tu wa wanajeshi hao huku magoli kadhaa ya wazi yakikoswa na wagosi hao,wachezaji waliokosa magoli katika kipindi cha kwanza ni Obright Obinna mawili na Utugi moja na Masumbuko moja.Baada ya timu kwenda mapumziko kocha wa wagosi yusuph Chipo alifanya mabadiliko ya kimfumo kwa kumuingiza katikati ya Uwanja Mahundi na kumpeleka pembeni Itugi hivyo kuwa mwiba mchungu kwa Wanajeshi hao kwa dakika nyingine 45 za mchezo.
| |
| Mashabiki wakiwazonga Mbeya City na Kuwapisha Mgambo |
Coastal ilijipatia bao kupitia Itugi baada ya kutokea Gonga safi upande wa wanajeshi hao. Goli hilo liliongeza kasi ya Coastal Union kwani walikosa magoli kadhaa kupitia Mahundi ambaye alitoka nje baada ya mchezo akiwa anaburuzwa kwa kilio kwa kukosa magoli mengi ya wazi.Mashabiki walikuwa na hamasa kubwa mno na baada ya mchezo walianza kuwafuata Mbeya city na kuwaambia watakufa kwa Mgambo leo.Msemaji wa Ruvu shooting Masau Bwire alikuwa na wakati mgumu sana kwa mashabiki wa Wagosi baada ya kuongea sana kabla ya Pambano na watu walitaka aongee tena.Kila l kheri Mgambo Shooting leo dhidi ya Mbeya City
 |
| MASHABIKI WAKIENDELEA kUFURAHIA USHINDI |
 |
| Mfungaji wa Goli la Coastal |
 |
| Coastal wakitoka Kushangilia Goli lao |
No comments:
Post a Comment