wakati nikiwa na harakati za kutaka kucheza mpira nilianza kucheza kama Beki wa kulia na kitu kimoja kilichoniondoa huko ni Kadi za mara kwa mara, miguu yang haikuwa ikirudi nyuma nitakapoifyatua nikikosa Mpira nakusomba wewe, Nguvu haikuwa tatizo miguuni mwangu sasa marefa walikuwa wanatafsiri vibaya
mchezo wangu huo. Baada ya kupewa kadi nyekundu mbele ya umati wa watu pale katika Dimba la
Mkwakwani na aliyekuwa Refa wa FIFA wakati huo Marehemu Bakari Mtangi nilikata Shauri la kuhama namba nakucheza mbele lengo likiwa ni kuwa mimi nakabwa sio kukaba, Moja ya zoezi la kucheza Striker lililokuwa linanishangaza ni kufunga goli pasipo na kipa,Kocha anawapanga timu mbilihalafu anawaondolea makipa ili mufunge Kirahisi lengo Ni kuwazoezi kufungaSikulipenda kwani niliona kama anatudharaunilitaka aweke kipa anitambue kwa Mashuti yangu,baadae sana nilikuja kuelewa somo hasa baada ya mimi kusomea ukocha..
![]() |
Marcio Maximo akimpa Maelezo JAJA |
Lengo ya kastory hako ni kuwa Ufungaji wa Magoli,ama kuweza kufunga hakuhitaji Ugumu ama Urahisi wa Ligi,anayeweza Kufunga anafunga tu haijalishi Ligi hiyo inachezwa na Maroboti ama Chochote yeye atafunga tu na Kocha hana shaka na mtu ajuaye kufunga,TazamaMarcio maximo alivyopata taabu ya
![]() |
Kocha mkuu wa Young African Marcio Maximo |
lielewa tatizo la Watnzania ama wana Yanga ni kufunga,Wapo kina Coutinho wengi sana Brazil lakini Kina JAJA Nao wapo japo ni wachache na sitegemei kwa Kocha mwenye Ueledi kama Maximo alimleta Jaja kwa Bahati mbaya Kumpendelea kwa kuwa ni brazil mwenzake.
![]() |
Coutinho |
Mambo watu wameyaona wenyewe na uwezo wake umeonekana na mara zote wafungaji wazuri wakifunga utafikiria kabahatisha ama kafunga Goli rahisi lakini nenda wewe uone kazi ya kulifunga hilo goli,,Shikamoo Maximo..Salute Jaja..keep on MALAPA.
Tukielekea kule kwenye ligi kuu ya soka England..siku zote wadau ama wapenzi wa soka wamekuwa wakisema mtu kama Messi akienda England hawezi kufunga kutokana na Ugumu wa ligi hiyo Si kweli na hili limethibitishwa na Diego Costa pale Chelsea..Mourinho anajua anataka nini,baada ya ligi kuu kuisha tu alichokifanya ni Kumnunua Costa bila kuchelewana kuwaondosha Lukaku,Torres,Demba Ba na Eto
ili kumpisha Diego Costa mmoja tu,,hapa ndio narudia
![]() |
Jose Mourinho |
muda wake wa kucheza pale yeye aliona hapana,Matunda ya Costa yameonekana Mechi Nne magoli saba peke yake, Kama kuna sehemu ambayo makocha wanaishindwa kuifundisha ni sehemu ya Ufungaji basi..Zile mbinu za kuacha goli wazi ni kama Majaribio tu na kuwapa watu mazoea ya kufunga kinguvu hususani wafungaji wa kuunga unga ila hawa wa Kariba ya kosta nafikiri wanatakiwa kuwekew makipa wawili zaidi ili kuwapa ugumu wa kufunga mazoezini na wakapate wepesi wa kufunga kwenye Mechi
kama afanyavyo..Shikamoo Mourinho..salute Diego Costa
No comments:
Post a Comment