Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Friday, December 4, 2015

Neymar (1)
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar amesema kuwa anatarajia kuongeza mkataba wake katika timu yake ya sasa ya Barcelona kwani ndio sehemu anataka kuendelea kubaki kuchezea pamoja na uwepo wa changamoto ndogondogo zinazomkabili.
Tayari baba mzazi wa Neymar, amemtaka mchezaji huyo kutokimbilia kusaini mkataba na klabu ya Barcelona hadi hapo litakapomalizwa suala la matatizo ya ukwepaji wa kodi katika usajili wake.
Lakini pamoja na kauli hizo za Neymar Snr. mchezaji huyo amesema anahitaji kuongeza mkataba na timu hiyo kwani ndio sehemu anataka kuendelea kucheza mpira.
Neymar bado ana miaka kadhaa katika mkataba wake unaoisha 2018 lakini amesisitiza kuwa na furaha klabuni hapo huku akiwa ni figure muhimu katika kikosi hicho na nyota sasa ni ya kijani kwa mchezaji huyo kushinda tuzo ya Ballon d’Or siku za usoni.

huyu Ndio mchezaji anayesumbua kwa sasa kule ENGLAND

vard 1vardvard2vard3

Monday, November 30, 2015

Madrid Wafuta Machozi ya Barcelona


Eibar: Riesgo, Capa, Pantic, Dos Santos, Junca, Escalante, Dani Garcia, Adrian (Verdi 69 mins), Saul Berjon, Inui, Enrich (Arruabarrena 86)
Subs not used: Irureta, Ramis, Silvestre, Harjovic, Luna
Booked: Dos Santos, Escalante

Real Madrid: Navas, Carvajal (Benzema 85), Nacho, Pepe, Danilo, Kroos, Modric, Kovacic (Casemiro 79), Rodriguez (Lucas Vazquez 65), Bale, Ronaldo
Subs not used: Casilla, Arbeloa, Cheryshev, Lazo
Goal: Bale 43, Ronaldo pen 82











Arsenal Yachechemea...Alex sanchez majanga

Kipute cha Ligi kuu ya soka ya Uingereza kiliendelea Jana
kwa Arsenal kutoa sare ya Goli moja kwa Moja na Norwich
katika mchezo mgumu na wa kusisimua,,Mchezo huo
ulishuhudia Mchezaji tegemeo wa Arsenal Alex SANCHEZ
Akiumia.
NORWICH 4-2-3-1: Ruddy 5; Wisdom 6.5, Bennett 7.5, Bassong 6.5, Olsson 6.5; O’Neil 6.5, Dorrans 6; Howson 6 (Redmond 71, 6), Hoolahan 6 (Odjidja-Ofoe 85), Brady 6.5; Grabban 6.5 (Jerome 85).
SUBS: Rudd, Martin, Mulumbu, Mbokani.
BOOKINGS: O’Neil.
MANAGER: Alex Neil 7.

ARSENAL 4-2-3-1: Cech 6.5; Bellerin 6, Mertesacker 6, Koscielny (Gabriel 11, 5), Monreal 7; Flamini 6, Cazorla 6; Ramsey 6 (Oxlade-Chamberlain 71, 5), Ozil 665, Sanchez 6 (Campbell 61, 5); Giroud 5.
SUBS: Ospina, Debuchy, Chambers, Reine-Adelaide.
BOOKINGS: Cazorla
MANAGER: Arsene Wenger 6.
MOM: Ryan Bennett
REF: Jon Moss 6.

ATT: 27,091.

Wednesday, September 30, 2015

Arsenal Ni ya Mchangani tu

 Timu ya soka ya Arsenal ya England jana iliangukia Pua
katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kupokea
kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa wagiriki
Olympiakos.
 Hiyo ni mechi ya pili kwa Arsenal kufungwa katika ligi
hiyo huku ikishuhudiwa pia waingereza
wenzao Chelsea wakilala Ugenini kwa Fc Porto kwa
Idadi hiyo hiyo hiyo ya mabao.
 Leo Mashetani wekundu watapambana na Wolsburg
katika muendelezo wa ligi hiyo katika Uwanja wa OLD
Trafford


Monday, September 21, 2015

Wagosi wa Kaya Wafungua kwa Point Moja

Timu ya soka ya Coastal Union ya Tanga almaarufu
Wagosi wa Kaya jana walishindwa kuutumia vema
uwanja wao wa Nyumbani Mkwakwani katika mechi
ya vuta nikuvute wa Ligi kuu ya soka Tanzania bara
baina yao na TOTO Africans ya mwanza.Katika
mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi wa
kizungu ulikuwa mkali na mashambulizi ya kushtukiza
kwa kila Upande.Timu hiyo ya Coastal union ilipata
vichapo katika mechi mbili zilizopita kati yao na Yanga
na Ndanda F.C ,Ligi hiyo itaendelea tena katika uwanja
wa Mkwakwani kwa Mechi kati ya Coastal Union na
 Mwadui ya Shinyanga inayonolewa na Jamhuri Kihwelo
(JULIO)Aliyewahi kuionoa Coastal Union msimu uliopita.
na Jumapili kutakuwa na Mchezo kati ya African Sports
na NDANDA F.C Ya mtwara.

Sunday, September 20, 2015

NGOMA WA YANGA AJINASIBU

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amesema mechi dhidi ya Simba, itakuwa kama mechi nyingine na ana uhakikaa atafunga.


Ngoma raia wa Zimbabwe, amefikisha mabao matatu katika mechi zake tatu za Ligi Kuu Bara. Mechi ya nne ni dhidi ya Simba, wikiendi ijayo.

"Nimeanza kuona ugumu wa ligi, lakini ninaona pia napata uzoefu na kujua cha kufanya. Simba ni watani wa Yanga lakini ni timu kama nyingine.

"Kufunga hakuwezi kuwa asilimia mia, lakini ninaamini uwezo wangu, ninawaamini wenzangu na ninaiamini timu kwa ujumla na ushirikiano wetu.

"Litakalotokea kama ni kufunga au kutoa pasi, lakini kikubwa Yanga ishinde ili twende na mwendo huu," alisema Ngoma