Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Thursday, January 8, 2015

Gerard Athibitisha Kuhamia L.A Galaxy

Steven Gerard
Nahodha na Mchezaji wa timu ya Taifa ya England Steven Gerard
amethibitisha kujiunga na Timu ya L.A Galaxy mwishoni mwa Msimu
huu baada ya awali wiki hii kutangaza rasmi kuacha kuchezea timu
yake ya utotoni Liverpool.Akitangaza hatima yake hiyo Gerard
alisema kuwa Asingependa kucheza ulaya kwani kungekuwa na
uwezekano wa kukutana na timu yake hiyo ya zamani katika mechi
jambo ambalo hakupenda Litokee.Nina furaha sana kuanza hatua
mpya ya maisha yangu ya soka pengineko baada ya kukaa Liverpol
kwa muda wote wa maisha yangu ya soka.L.A Galaxy ni timu kubwa
sana ya soka hapa Marekani,mazungumzo yangu na Kocha Bruce
Arena pamoja na mkurugenzi wa timu yalikuwa ya kusisimua.
Nitajitolea kuisaidia L.A.Galaxy kushinda mataji lakini kwa Muda
huu nikiwa bado Liverpool nitajitoa mpaka dakika ya mwisho ili
kufanikisha lolote linalowezekana.Kocha wa Galaxy Bruce Arena
amesema tuna bahati sana kuwa na mchezaji wa kiwango cha
Steven Gerard,Ni mchezaji wa kidunia na atakuja kwetu akiwa na
utajiri wa Uzoefu na mataji,atakuwa chachu ya wachezaji wetu
wachanga.

No comments:

Post a Comment