| Wachezaji wa Mgambo |
| Wachezaji wa Mgambo wakisikiliza Mwalimu |
| African Sports |
| African Sports |
| Mchezaji wa African Sports Mussa Chambe |
ya mjini Tanga leo imewapa wapenzi na mashabiki
wake raha baada ya kuwafunga Mgambo shooting
ya kabuku handeni Tanga.Mchezo huo wa kirafiki
ulikuwa na lengo la kuzipa mazoezi timu zote hizo ktk
michezo ya ligi kuu ya Soka ya Vodacom kwa Mgambo
na ligi daraja la kwanza kwa African Sports.Goli la
kwanza la African Sports limefungwa na kiungo wake
Alli Kagawa baada ya Uzembe wa Golikipa wa Mgambo
katika dakika ya kwanza.Mgambo waliamka na kutaka
kuswazisha bao hilo na kunako dakika ya 25 walifanikiwa
kufunga goli lakini muamuzi wa pembeni aliashiria kuwa
ni Offside,mpaka mapumziko Mgambo 0-African sports1
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku African sports
kuonekana kuchoka sana sababu ya kukosa mazoezi,
Lakini ilikuwa African Sports tena waliojiandikia Goli la
pili katika dakika ya 90 ya mchezo huo kupitia kwa
Mendy baaada ya makosa ya mabeki wa kati wa Mgambo
kujichanganya wenyewe.Mechi hiyo ilishuhudia African
Sports wakimtambulisha mchezaji wao ALI SHIBOLI
Kwa mara ya kwanza tokea wamsajili pamoja na PAULO
RASTA..Wakati Mgambo waliwatambulisha Agoye
na Sebarua.

No comments:
Post a Comment