Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Friday, December 26, 2014

Balotelli Bado anahangaika Kuzoea Aina ya Mchezo Wa Liverpool..Rodgers

Kocha wa Liverpool Brendan Rogers amekaririwa akisema kuwa
Mario Baloteli anahangaika kuweza kumudu Mchezo wa Liverpool
mpaka sasa.Mchezaji huyo atakuwa safarini kuelekea Turf Moore
japokuwa kuna uwezekano akaanzia Nje katika pambano hilo la leo.
Balloteli anajumuishwa kwenye kikosi baada ya kumaliza adhabu ya
kutokucheza mechi moja kutokana na maneno ya kibaguzi,Mchezaji
huyo mwenye asili ya Ghana anayekipiga katika timu ya taifa ya Italia
hajafunga hata goli moja katika ligi kuu huku akiwa na goli moja tu
kwenye mashindano mengine.Rodgers amebadili mfumo wa timu kwa
sasa na kuwa 3-4-3 ambao amesema Balloteli hawezi kufiti katika
mfumo huo.Mfumo huo ni mahususi kwa Kiungo wa Uingereza anayeng"aa
kwa sasa Raheem Sterling.

No comments:

Post a Comment