Mgosi wa Sui

Mgosi wa Sui

Thursday, October 23, 2014

Wagosi wa Kaya Wapaa kuelekea BUKOBA

Timu ya Soka ya Wagosi wa kaya Coastal Union"Mangushi"
Leo kunako majira ya saa tisa alasiri wamepaa kutoka Uwanja
wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere kuelekea
mjini Bukoba kwa kupitia Mwanza kwa Ndege ya Shirika la
Ndege la Fastjet.Timu hiyo imeondoka na Wachezaji wake
wote kwa ajili ya Mchezo wa ligi kuu ya soka ya Vodacom
kati yao na Kagera Sugar ya Mjini huko,Ieleweke wazi kuwa
moja ya timu chache inayotumia Usafiri wa Anga nchini ni
Wagosi wa kaya Coastal Union kwa Mechi zote zinazochukua
zaidi ya siku nzima kwa Basi wao hutumia Ndege ili kutowachosha
wachezaji wao,Wakati huo huo Timu nyengine kutoka Tanga
Mgambo Shooting Imewasili mjini Mtwara leo kwa ajili ya
maandalizi ya Mchezo dhidi ya Ndanda FC Ya mjini huko,
Timu hiyo ya Ndanda ambayo itakuwa mwenyeji wa Mgambo
juzi walimtimua Kocha wao Kitambi kwa Matokeo mabovu
mfululizo,Timu hizo zitapambana Jumamosi hii.KILA LA
KHERI WAGOSI,KILA LA KHERI,MGAMBO

No comments:

Post a Comment